Mfumo wa kidijitali wa usimamizi wa maji ulio rahisi, bila malipo na unaoweza kufanyiwa mabadiliko
Simamia mfumo wako wa maji, mfumo wa kutupa maji taka, mita za kidijitali na mengine zaidi
Ungependa kuwa wa kwanza kutumia Qatium?
Kabla ya kujisajili tafadhali thibitisha kwamba unakubaliana na sheria na masharti
Maelezo ya msingi kuhusu Ulinzi wa Data
Mdhibiti wa Data: Qatium (Deep Tech Solutions S.L.)
Nia: Ili kukutumia machapisho, matangazo ya bidhaa na / au huduma na bidhaa zinazotengenezwa tu na Qatium.
Msingi wa Kisheria: Idhini yako.
Wapokezi wa data: Data utakazotupatia zitahifadhiwa kwenye seva za Active Campaign (mtoa huduma za matangazo ya barua pepe) kupitia kampuni lake la ActiveCampaign, Inc. lililoko nchini Marekani na lililoungwa mkono na mfumo wa Ngao ya Faragha kati ya Umoja wa Ulaya na Marekani.
Haki: Una haki ya kufikia, kubadilisha, kudhibiti na kufuta data kupitia [email protected], pamoja na haki ya kuwasilisha lalamiko kwa mamlaka ya usimamizi.
Maelezo ya ziada: Unaweza kuangalia habari zozote za ziada na zenye maelezo ya kina kuhusu Ulinzi wa Data katika sera yetu ya faragha.
Fahamu nguzo za mfumo wetu
Piga jeki mabadiliko ya kidijitali ya kampuni lako bila kujali kiwango chako cha ujuzi au data
Ni rahisi
Ni programu yenye akili bandia iliyo rahisi kwa mtumiaji
Kisaidizi chetu ni kiwezeshi kinachotumika kote ulimwenguni kinachokupa mwongozo katika mchakato mzima wa usimamizi wa maji. Utaweza kufanya maamuzi bora zaidi kwa ajili ya mfumo wako bila kujali ujuzi ulio nao. Mfumo wetu hujifunza kutoka kwa mifumo yote ya maji, hivyo basi kuboresha mfumo wako, na pia unaweza kusoma fomati za GIS, kwa kuwezeshwa na akili ya mashine.
Haulipiwi
Hakuna vizingiti wala mipaka
Qatium ni teknolojia mpya ya mfumo wa usimamizi wa maji. Unaweza kuipata moja kwa moja kwenye kivinjari chako na huhitajiki kusakinisha programu zilizo gumu kutumia, zinazoingilia faragha yako au za bei ghali. Mfumo huu hukupa habari unazohitaji ili kutumia rasilimali zako kikamilifu na kupata manufaa mengi zaidi kutoka kwa mfumo wako wa maji bila mali malipo, hivyo basi kuufanya thabiti zaidi, huku ukitumia nguvu kidogo ya nishati na haidroliki.
Ni mfumo wazi
Jamii inayoshirikiana na kuhusisha wote
Mfumo wetu umeimarishwa na ujuzi katika nyanja mbalimbali na mazingira ya wataalamu kama vile wabunifu, wataalamu wa haidroliki na washika dau wengine muhimu – huku wote wakishirikiana kufanya ubunifu kwa pamoja ili kusuluhisha tatizo la usimamizi wa maji na kuongoza katika mabadiliko ya kidijitali kwenye sekta ya haidroliki. Umekaribisha kushirikiana nasi!
Faida na manufaa ya ziada
Mwamko mpya wa kidijitali
Geuza mfumo wako mkuukuu wa maji kuwa mpya na wa kisasa kwa njia rahisi
Uthabiti / Usuluhishaji wa matatizo
Kuwa tayari kwa matatizo yanayoweza kuibuka kutokana na kisaidizi chetu
Utumizi mzuri wa nishati na nguvu ya haidroliki
Pata manufaa kamili kutoka kwa rasilimali zako ili kupata mfumo wa maji wenye gharama ndogo
Mfumo wa moja kwa moja
Qatium ni mfumo wa moja kwa moja ambao unaendelea kukua. Tunaanza siku ya leo kwa kukusaidia katika mfumo wako wa maji, lakini hilo sio jambo la pekee tunaloweza kukusaidia nalo! Mwezi baada ya mwingine, tutakuwa tunatoa masalio ya teknolojia yetu, hivyo basi usiachwe nyuma!
Toa mchango wako katika kuboresha mustakabali wa ulimwengu kwa kupiga kura na kutoa maoni yako kuhusu malengo yetu.
Yanayokuja karibuniBaadhi ya wabunifu wengi tunaoshirikiana nao
Hassan ni mtaalamu tajika wa masuala ibuka ya usimamizi wa rasilimali maji, aliyebobea katika masuala ya usalama wa maji mijini. Ni mtafiti wa daraja la uzamivu katika Chuo Kikuu cha Ufundi cha Cologne (TH-Köln) wa masuala ya usimamizi wa rasilimali maji zilizounganishwa na usalama wa maji mijini. Yeye pia ndiye Naibu Rais wa Baraza la Maji la Mashariki ya Kati (MEWF) na mwanachama hai katika makundi mengi ya kimataifa ya masuala ya maji na hali ya anga.
Among other activities, he is a Governor’s appointee to California’s Bay Delta Vision Blue Ribbon Stakeholders Committee, a Board member on the California Climate Action Registry and a member of the UCLA Continuing Education Sustainability Advisory Board.
Ni mwandishi wa kitabu kilichouzwa sana; mtafiti mkuu katika fani ya vita vya uasi na vya misituni, na pia ni mwanajeshi mtaalamu aliyestaafu na mwanadiplomasia. Anatoa ushauri kwa taasisi za kimataifa, serikali, biashara, mashirika yasiyo ya kiserikali na jamii za kieneo kote ulimwenguni, huku pia akishughulikia changamoto changamano za masuala ya ubinadamu na usalama barani Afrika, Mashariki ya Kati, Amerika ya Kusini na Asia.
Ni mwanazuoni tajika wa masuala ya mikakati ya maji na ubunifu anayetambulika kote ulimwenguni. Ameandika vitabu na makala mengi na kuwasilisha mada za: thamani ya maji, ubunifu katika teknolojia ya kidijitali ya maji, uchumi duara, na uhusiano wa nishati, maji na chakula.
Amebobea katika utafiti unaoangazia taaluma anuwai ya utatuzi wa masuala ya maji kupitia teknolojia habari, ambao unavuka desturi za kawaida za sayansi za maji/mazingira, sayansi ya habari/sayansi ya kompyuta (ikijumuisha Akili Bandia, uchimbaji wa data na mbinu za kuhakikisha matumizi kamilifu) na uhandisi wa mazingira.
Kichwa cha utafiti wa hivi punde zaidi ni Matumizi ya Maji Zaidi ya Mara Moja na Upatikanaji wa Maji: Mtazamo Mpya wa Kusimamia Rasilimali Maji, uliozingatia dhana za Usalama wa Maji na Uchumi Duara zinazotumika katika fani hii. Pia yeye ni mwanzilishi wa Deságue, ambayo ni podkasti ya nchi ya Brazil inayozungumzia mahusiano ya sayansi ya maji, siasa na jamii.
Kuangaziwa kwa hivi karibuni kwa kuchakatwa kikamilifu kwa maji ya maziwa, ikijumuisha kuondolewa kwa chumvi kwa hali ya juu pamoja na kuzalishwa kwa madini na kemikali (ZLD). Gavin amebuni Mkakati wa Kuanzisha Miji Janja Mipya kwa mtazamo wa Miji huku ukitilia maanani shughuli zote za Mashirika ya Maji.
Muhtasari wa mfumo

Hatua ya 1
Kijenzi cha Mfumo
Ikiwa hauna za Kijiografia (GIS) Mfumo wa Habari au hauna data zingine, Qatium itakuruhusu kubuni mfumo wako kutoka mwanzo, kwa kuchora vipengele vyako vya mfumo au kwa kutumia violezo vya mifumo vilivyoandaliwa awali.
Hatua ya 2
Faili ya GIS
Mfumo wetu utakupa mchakato rahisi wa kupakia Mfumo wa Habari za Kijiografia (GIS) na kutambua kila kipengele kwenye mfumo wako, na kuambatana na mabadiliko ya kiotomatiki ya kitopolojia, muundo wa haidroliki na mengine zaidi!


Hatua ya 3
Miundo inayotumia haidroliki
Huhitaji kuwa mtaalamu ili kutumia mfumo wa Qatium. Ikiwa hujui jinsi ya kukamilisha moja ya sehemu hizi, kisaidizi chetu cha mtandaoni ili kukuongoza kwenye mchakato huo, na kuweka mipangilio ya muundo kiotomatiki kwa niaba yako.
Hatua ya 4
Mitazamo
Utapata mtazamo bandia wa utendakazi wa mfumo wako wa awali, wakati uliopo na wakati ujao. Mfumo huo utalinganisha data halisi na data bandia.


Hatua ya 5
Kifanya maamuzi
Qatium itakusaidia kufanya maamuzi bora zaidi kwa kukuonyesha hali. Mfumo wetu utaboresha usimamizi wa mfumo, na kukupa habari muhimu zinazohitajika ili kuweza kutabiri matatizo yanayoweza kutokea kwa ajili ya kuchukua hatua zinazofaa.