Inawezekana kwamba maji ya chupa ni mojawapo ya hila kuu zaidi za uuzaji katika karne iliyopita. Matangazo hutuambia kwamba maji yao yana afya njema zaidi, yana ladha nzuri, pamoja na manufaa mengine ya kutiliwa shaka. Kwa sababu ya matangazo, hatufahamu ikiwa tunafaa kununua maji ya chemchemi, maji yenye madini au maji ya kawaida ya chupa.

Hila Hizi Huweza Kutushawishi Vipi?

Masoko ya maji ya mfereji na yale ya chupa yatashindania kupata ushawishi mkubwa ulimwenguni utakaoyapa manufaa makuu ya kifedha. Hali hii mara nyingi husababisha migogoro kati ya wananachi wanaopokea habari za uongo, kwa sababu hawafahamu tena kuhusu ni habari zipi za kweli na ni zipi za uongo. Kando na hilo, tunafaa kutilia maanani athari kwa mazingira.

Hali hii inakinzana na ukweli kwamba watu wanaotumia maji ya chupa sana wanatoka mataifa yenye maji safi ya kunywa. Watu hawa hawana imani na maji ya mifereji, ingawa hawana sababu tosha za kuyatilia shaka.

Huenda sababu moja ikawa ladha ya maji ya mifereji katika maeneo mengine. Lakini hoja hii hairidhishi tukizingatia gharama ya juu ya maji ya chupa kwa uchumi na mazingira. Aidha, baadhi ya tafiti za kuonja maji bila kufahamu aina yayo zinaonyesha kwamba mara nyingi, hatuwezi kutambua tofauti kati ya ladha ya maji ya mfereji na ya chupa.

Wakati mwingine, ladha “mbaya” ya maji ya mfereji kutoka maeneo mengine husababishwa na jiolojia ya ardhi hiyo. Maji hupitia safu tofauti kabla ya kusafishwa, kama vile udongo wenye jipsamu na chumvi, pamoja na viwango tofauti vya ugumu au kuwa na klorini. Ladha hii kamwe haifai kuhusishwa na hatari za kiafya. Maji ya kunywa huwa chini ya masharti na udhibiti mkali. Kamwe hayazidishi viwango vya usalama vilivyowekwa na mashirika ya kimataifa kama vile Umoja wa Ulaya au Shirika la Afya Duniani (WHO). Maji ya kunywa ni mojawapo ya bidhaa za kuliwa na kunywewa zilizo chini ya udhibiti wa juu sana.

Uchafuzi wa Mazingira na Plastiki

Ikiwa dosari kubwa zaidi ya maji ya mfereji ni ladha yake, uchafuzi ndio dosari kubwa zaidi ya maji ya chupa. Hatufahamu kiasi cha plastiki kinachotengenezwa kote ulimwenguni. Sehemu kubwa ya kiasi hicho huchangiwa na maji ya chupa. Huenda tukadhani kwamba kurudufu plastiki kunatosha, lakini plastiki haiwezi kurudufiwa kikamilifu (tofauti na gilasi au alumini). Sharti pia tukumbuke kwamba mchakato wa kurudufu hutumia kawi na unachafua. Kwa sababu hii, hatua inayofaa ni kupunguza matumizi ya plastiki iwezekanavyo.

Nchi ambazo maji ya chupa yanatumika zaidi ni zile zenye ustawi mkubwa kiasi kwamba zinaweza kuhakikishia raia wake ufikivu wa maji ya kunywa

Kisaidizi Bandiacha Qatium

Uchafuzi Mkubwa Unaosababishwa na Utengenezaji wa Plastiki

Utengenezaji wa chupa ya plastiki hutumia petroli (kama mali ghafi na pia ili kutoa kawi) pamoja na mafuta mengine ya kisukuku, lakini pia hutumia maji (kati ya galoni .26 hadi .52 kwa kila chupa). Mwishoni mwa mchakato wa utengenezaji, sharti pia tuzingatie rasilimali zilizotumika katika usafirishaji na usambazaji.

Kwa upande mwingine, hatuthamini uwezo mkubwa wa usafirishaji wa mifumo ya usambazaji ya maji ya mfereji, ambayo husafirisha maji kwa kutumia kawi ya kiwango kidogo.

water-tap

Maji ya Mfereji

Dosari nyingine ni bei ya maji ya chupa. Hata hivyo, si tatizo kwa watu wengi kutumia pesa nyingi kununua maji ya chupa kuliko zile wangetumia kununua maji ya mfereji. Huenda bei ya maji ya chupa ikaonekana kuwa chini, lakini kwa familia ya wastani, inaweza kufika mamia ya dola kwa mwaka. Cha kushangaza ni kuwa, lita moja ya petroli kabla ya kutozwa kodi hugharimu pesa kidogo kushinda galoni 0.26 za maji mengine ya chupa.

Huku tukizungumzia kodi, tunafaa kujiuliza ikiwa maji ya chupa (na bidhaa zote zinazofungwa kwa plastiki kwa jumla) yanafaa kutozwa kodi maarufu ya kaboni. Nchi nyingi tayari zinatoza kodi hii kwa bidhaa zingine za matumizi ya kawaida.

Hatimaye, huenda suala la maji ya mfereji na maji ya chupa likageuka kuwa mojawapo ya mashindano makali zaidi ulimwenguni, kama vile—kati ya kompyuta za Mac na PC? Maradona au Pele? Kechapu au kachumbari? Cha kusikitisha ni kwamba, kampeni nzuri ya kufanya mauzo huenda ikaaminiwa zaidi ya mwanasayansi bora zaidi ulimwenguni.