Kila mwaka, takriban watu milioni moja hufariki kwa sababu ya kukosa maji safi. Wanaoathirika zaidi ni watoto na wakongwe. Maana yake ni kwamba karibu watoto elfu moja wanafariki kila siku kutokana na magonjwa yanayohusiana na maji machafu. Kutengeneza mfumo wa kutoa maji unaosimamiwa vyema, pamoja na mifumo ya kutupa taka isiyotumia maji kutaboresha pakubwa hali ya maisha ya zaidi ya watu milioni 700. Watakaofaidika zaidi ni wale wasioweza kupata chanzo cha kudumu cha maji safi.

Maji Yanayopotezwa

Maji yasiyo na chumvi ni rasilimali asili iliyo muhimu sana katika kusitiri maisha, lakini kufikia mwaka wa 2025, huenda nusu ya idadi ya watu ulimwenguni watakuwa wakiishi katika maeneo yenye uhaba wa maji. Sasa hivi, miji mingine hupoteza maji kwa kiasi cha zaidi ya asilimia 50. Hii inaashiria kupoteza kwa rasilimali hii muhimu kwa kiasi kikubwa. Ukosefu wa usimamizi unaofaa husababisha maji kupotezwa kwa kiasi kikubwa. Kando na hilo, rasilimali nyingi zinazohitajika ili kusafisha vyanzo vya maji na mifumo ya kutupa maji na taka hupotezwa. Hivyo basi, ni muhimu sana kuwa na upimaji sahihi na endelevu wa mifumo ya maji. Hii inahakikisha kwamba maji yanasimamiwa ipasavyo, hivyo basi kupunguza asilimia ya maji yanayopotezwa.

water-networks-lowers-access

Tatizo la Maji Yanayopotezwa 

Kiwango cha maji kisichoonekana kwenye vipimo vya mita ni tofauti ya kiasi cha maji kinachoingia kwenye mfumo na jumla ya vipimo vyote vya mita. Kama mifumo haingekuwa na dosari, nambari hiyo ingekuwa sifuri. Hata hivyo, hali hiyo haitokei hasa kwa sababu mbili:

Kwanza, ni kwa sababu ya hitilafu katika upimaji. Pili, ni kwa sababu ya maji yanayovuja kwenye mfumo.

Maendeleo ya kiteknolojia yamesaidia kupunguza hitilafu za vipimo vya vihisi. Lakini kwa upande mwingine, uvujaji wa maji kwenye mifumo ya usambazaji husababishwa na kutotunza mifumo hiyo. Ni muhimu kukarabati sehemu za mifumo hiyo. Mifumo ya maji yenye shinikizo la juu huenda pia ikavuja maji. Kuna uwezekano mkubwa wa kuboresha mifumo hii na kupunguza kiasi hiki cha maji yasiyoonekana kwenye vipimo vya mita.

Kwa kifupi, kiwango cha maji kinachopotea kwenye mfumo hutegemea yafuatayo:

 1. Umri wa Bomba
 2. Shinikizo Kwenye Mfumo
 3. Mabadiliko ya viwango vya maji kwenye mfumo ya kila siku
 4. Vihisi vilivyowekwa kwenye mfumo
 5. Muda unaochukuliwa ili kutatua uvujaji na wasimamizi
 6. Miunganisho haramu

Hivi sasa, kuna mifumo ya usambazaji wa maji katika miji mingine ambayo inapoteza zaidi ya asilimia 50 ya maji yayo

Kisaidizi Bandiacha Qatium

Mkakati Wa Kuzuia Kupotezwa Kwa Maji

Ni muhimu sana kupendekeza mkakati mzuri wa kusuluhisha kupotea kwa maji. Ili kutatua shida hii, tunapendekeza maswali yafuatayo:

 1. Ni kiasi gani cha maji kinachopotea? Ni muhimu kukokotoa kiasi cha maji kinachosalia kwenye mfumo. Kiasi hicho ni tofauti ya maji yaliyoingia kwenye mfumo na yale yaliyorekodiwa kwamba yalitoka kwenye mfumo.
 2. Maji yanapotelea wapi? Ukaguzi wa mfumo utasaidia kutambua maeneo yanayovuja maji. Katika wakati huu, ni muhimu sana kwamba mfumo una vihisi vya kutambua kunakovuja maji. Pia kuchakatwa kwa data ni muhimu. Suluhisho hilo linafaa kuchukua muda mfupi sana. Kwa kufanya hivyo, tunapunguza maji yanayopotea.
 3. Kwa nini maji yanapotea? Kutambua sababu ya kupotea kwa maji hutusaidia kupata suluhisho la tatizo hilo. Kwa sababu hii, ni muhimu kuwa na ujuzi mpana wa mfumo unaosimamiwa.
 4. Ni nini tunachoweza kufanya kuzuia kuvuja kwa maji? Ni muhimu kuwa na mkakati thabiti wa kudhibiti uvujaji wa maji ili kuchagua suluhisho linalofaa la tatizo hilo. Kufanya utafiti kwa kuigiza hali halisi kutatuwezesha kutambua suluhisho litakalofaa zaidi.
 5. Tutazuiaje tatizo hili kutokea tena katika siku zijazo? Baada ya tatizo hilo kutatuliwa, lengo jipya ni kulizuia. Ni muhimu kuendeleza mkakati dumishi na pia kudumisha ufanisi unaotokana na mkakati huo.
water-networks-pipe

Utunzaji wa Mabomba ya Maji

Hivi Sasa na Siku Zijazo

Ukusanyaji na uchanganuzi wa data ni muhimu ili kubuni mkakati unaofaa wa kupunguza uvujaji wa maji. Kuboresha na kupunguza gharama za kuweka vihisi (IoT) kutatupa fursa ya kupata ufanisi katika mambo mbalimbali. Pia kuna manufaa yanayotokana na maendeleo katika uchanganuzi wa viwango vikubwa vya data. Kuboresha mbinu za uchakataji kwa kutumia teknolojia ya akili bandia kunatupa maendeleo makubwa katika juhudu za kupunguza kupotezwa kwa maji. Kuna changamoto kubwa zilizo njiani, lakini tukiwa na zana zinazofaa, tunaweza kupata suluhisho la matatizo ambayo yanaonekana kuwa donda sugu kwa sasa.