Zaidi ya watu milioni 3 hufariki kila mwaka kutokana na magonjwa yanayohusiana na usafi wa maji. Hii inamaanisha kwamba mtu mmoja hufariki kila baada ya sekunde 10. Vifo vingi kati yavyo hutokea katika nchi zinazoendelea. Tunaweza kuzuia vifo hivyo virahisi bila kutumia rasilimali nyingi. Zaidi ya watu bilioni 2,2 hawana huduma zinazosimamiwa vyema za maji ya kunywa. Aidha, watu bilioni 4,2 pia hawapati huduma salama za kutupa maji taka.

Kunywa maji na/au ufe

Mamilioni ya wanawake na watoto wanalazimika kutembea kwa zaidi ya kilomita 10 kila siku ili kupata chanzo cha maji. Kulingana na Shirika la Afya Duniani (WHO), asilimia 85 ya visababishi vya magonjwa na vifo duniani huletwa na maji machafu. Vifo hivi vinasababishwa na ukosefu wa maji safi. Watu wengi hujipata katika mtanziko wa kuchagua kunywa maji machafu ili kuishi. Lakini maji haya yanaweza kuwaletea magonjwa yanayoweza kusababisha kifo. Unywaji wa maji machafu unaweza kusababisha matatizo mengi. Baadhi ya matatizo hayo ni kuendesha, utapiamlo, maambukizi ya minyoo ya chango au kichocho, miongoni mwa mengine.

water-quality-illness-disease

Kuboresha ufikivu wa maji ya kunywa na huduma za kutupa maji kuna uwezo wa kuzuia asilimia 9 ya magonjwa yote ulimwenguni. Hii itasababisha kuboreshwa pakubwa kwa hali ya maisha ya mamilioni ya watoto katika mataifa yanayoendelea. Wao ndio wanaoathiriwa zaidi na mifumo duni ya maji.

Maji yaliyochafuka

Shirika la Afya Duniani linabainisha maji yaliyochafuka kama maji “yenye sehemu zilizochafuliwa kiasi kwamba hayatimizi kiwango cha ubora kinachofaa ili kutumika katika hali yake ya asili.” Uwepo wa vitu kama vijiumbe maradhi, metali nzito au kampaundi zingine hupunguza usafi wa maji. Uchafuzi wa maji husababisha kupunguka pakubwa kwa maji ambayo tayari ni rasilimali haba.

Sababu kuu za tatizo la maji ni:

  1. Kutosafishwa kwa maji taka: Takriban asilimia 86 ya maji taka hutupwa bila kusafishwa kwa namna yoyote. Hali hii inasababisha hatari kubwa kwa watu wanaoishi katika maeneo hayo.
  2. Kuongezeka kwa halijoto: Katika halijoto za juu, maji yana uwezo mdogo wa kushikilia oksijeni iliyochanganyika na maji. Hii inasababisha vifo vya viumbe vingi. Pia inasababisha kupunguka kwa uwezo wa maji wa kujisafisha yenye ili kuondoa dutu zingine.
  3. Maji kutoka kwa mifumo ya kumwagilia mimea maji: Shughuli nyingi za kilimo zinahusisha matumizi ya viuadudu, sumu za mimea na mbolea kwa viwango vikubwa. Bidhaa zote hizi zina athari kubwa kwa usafi wa maji.
  4. Ukataji wa misitu: Kupungua kwa misitu kunachochea mmomonyoko wa udongo. Kunasababisha ongezeko la dutu katika maji.
  5. Uchimbaji wa madini: Maji mengi hutumika wakati chuma zingine zinachimbwa. Maji hayo yasiposafishwa, yanakuwa tatizo kuu kwa mfumo wa ikolojia.
  6. Umwagikaji wa mafuta: Shughuli za kuchimba mafuta husababisha uchafuzi wa maji mengi sana.

Asili ina uwezo wa kiwango fulani wa kuondoa dutu zingine. Ili kuzuia kuzidi uwezo huu, ni muhimu kutumia vituo vya usafishaji wa maji. Vinasaidia kuzuia kutupwa kwa maji yaliyochafuliwa kwenye mazingira kusikodhibitiwa.

Watu wengi hujipata katika mtanziko wa kuchagua kunywa maji machafu ili kuishi. Lakini maji haya yanaweza kuwaletea magonjwa yanayoweza kusababisha kifo.

Kisaidizi Bandiacha Qatium
water-quality-survival

Wanawake wa Kiafrika wakitembea huku wakibeba maji kwenye vichwa vyao katika kijiji kilicho karibu na mji wa Tanzania

Kwa jumla, utupaji wa dutu za kioganiki kwenye mto kuna athari zifuatazo:

Zoni ya uvunjaji wa bakteria: hii hutokea tu baada ya kutupwa kwa dutu hizo. Kiasi cha oksijeni kilichochanganyika kwenye maji kinaanza kupungua kwa kasi. Viumbe dhaifu zaidi vinatoweka na uvunjaji wa bakteria unaanza.

Zoni ya uvunjaji tendaji wa bakteria: viwango vya oksijeni vimo chini sana kiasi kwamba uvunjaji wa anerobi unafanyika. Hii inasababisha kutolewa kwa gesi na harufu mbaya.

Zoni ya kurejea kawaida : viwango vya oksijeni vinaanza kuongezeka. Viumbe changamano vinaibuka tena na maji yanakuwa safi.

Eneo la maji safi: ni eneo lenye usawa mzuri wa sifa za maji za kifizikali, kikemikali na kibiolojia.

Maji ndiyo uhai

Kila siku, mamilioni ya watu wanapambana na athari mbaya za kuishi katika mazingira yenye maji machafu. Ili kuzuia tatizo hili, ni muhimu kuhakikisha ufikivu wa huduma nzuri za maji safi ya kunywa na za kutupa maji. Ulipokuwa unasoma makala haya, watu 25 wamefariki kutokana na sababu zinazohusiana na usafi wa maji. Huu ndio wakati wa kuchukua hatua!