Bila maji, hakuna uhai, ama pengine maisha hayatakuwa kama tulivyozoea. Tunaishi kwenye sayari hii ambayo sehemu yake kubwa ni maji ya bahari, na kama ni ya kipekee kati ya anga za juu, ni kwa sababu inatimiza hali zinazohitajika ili kusitiri maisha. Seli zote, ikijumuisha za wanyama na mimea, huwa na kiasi kikubwa cha maji, cha takribani asilimia 75. Seli hizi huhitaji maji mengi ili kuendelea kuwa hai. Bila shaka, maji ni dutu muhimu sana ambayo huwa sehemu ya vitu vyote, na kuupa ulimwengu taswira tunayoona. Hivyo basi lazima tuzungumzie maji yanayotumika katika uzalishaji.

Kwa nini ni muhimu kufahamu kiwango cha maji kinachotumika kuzalisha bidhaa?

Maji yasiyo na chumvi ndiyo rasilimali asili inayotumika zaidi katika utengenezaji wa bidhaa tunazotumia kila siku. Lakini tunafahamu kiasi cha maji kinachohitajika ili kukuza vyakula hivi? Hapa ndipo dhana ya maji yanayotumika kuzalisha bidhaa inapoangazia na kuondoa shaka kuhusu kiasi cha maji kinachotumika kwa kila bidhaa.

Arjen Hoekstra na Mesfin Mekonnen, ambao ni watafiti katika Chuo Kikuu cha Twente (Uholanzi), walibuni dhana hii katika mwaka wa 2002. Lengo lao lilikuwa kuonyesha athari ya matumizi ya maji katika kutengeneza bidhaa tunazotumia kila siku, kwa kufichua viwango vya maji vinavyotumika.

Katika hali iliyopo tunaposhuhudia mabadiliko ya hali ya anga na ongezeko la watu, rasilimali maji zinatumika sana. Hii inamaanisha kwamba ufikivu wa maji yasiyo na chumvi unapungua kwa kiwango kikubwa bila kusita. Sasa hivi, ukosefu wa rasilimali maji huathiri watu 4 kati ya 10, na kufikia mwaka wa 2025, huenda tatizo hili likaathiri asilimia 67 ya watu ulimwenguni. Kwa sababu hii, tunahitaji kutambua umuhimu wa maji. Ni muhimu sana kupunguza matumizi ya rasilimali maji ili kuboresha uwezo wa kuiga maisha ya siku zijazo yatakayokuwa na changamoto.

Marc Burkley ni mwanachama wa Mtandao wa Wataalamu wa Uvumbuzi na Kilimo, Vyakula na Vinywaji wa Jukwaa la Uchumi wa Dunia na ni mmoja wa watetezi wakuu zaidi wa Malengo 17 ya Maendeleo Dumishi (SDG) ya Umoja wa Mataifa. Anasisitiza kwamba, “Maji ndiyo rasilimali yenye dhamani kuu zaidi ambayo tunayo”. Hii ni kwa sababu rasilimali hii huathiri malengo yote ya maendeleo dumishi kwa namna zilizo na zisizo za moja kwa moja. Kwa sababu hii, kusuluhisha matatizo yanayohusiana na ukosefu wa maji safi kunaweza kuboresha hali ya sasa ya malengo hayo yote.

Sasa hivi, ukosefu wa rasilimali maji
huathiri watu 4 kati ya 10,
lakini mnamo 2025, huenda tatizo hili likaathiri asilimia
67 ya watu ulimwenguni.

Kisaidizi Bandiacha Qatium

Tunawezaje kukokotoa kiasi cha maji kinachotumika katika uzalishaji wa bidhaa?

Maji yanayotumika kuzalisha bidhaa ni kiasi cha maji kinachotumika na/au kuchafuliwa katika hatua zote za uzalishaji. Hupimwa kwa vipimo vya ujazo (lita, mita za mchemraba, galoni…), ili kutupatia taswira ya athari ya bidhaa fulani juu ya maji yasiyo na chumvi. Hivyo basi, kiasi hicho huzingatia maji yanayotumika moja kwa moja katika uzalishaji, pamoja na matumizi yasiyo ya moja kwa moja ya maji yanayotumika kwenye mali ghafi ya bidhaa hiyo.

Kwa mfano, ikiwa tunataka kupima maji yanayotumika kuzalisha ratili 2 za nyama ya ng’ombe, huenda tusizingatie tu maji anayokunywa ng’ombe huyo, lakini pia maji yanayohitajika kuzalisha chakula chake pamoja na yale yaliyochafuliwa katika mchakato huo. Baada yake, huenda tukaongeza kiasi cha maji kinachohitajika kusafirisha nyama hiyo hadi kwenye supamaketi, maji yanayotumika kuihifadhi jokofuni, n.k.

Kategoria za Maji Yanayotumika Katika Uzalishaji Bidhaa

Kuna kategoria tatu zinazolingana na chanzo cha maji yaliyotumika katika kuzalisha bidhaa. Hili ndilo pendekezo alilotoa Profesa Hoekstra mwaka wa 2008 kuhusu Mfumo wa Maji Yanayotumika Katika Uzalishaji Bidhaa:

  • Maji ya kijani yanayotumika katika uzalishaji: haya ni maji ya uzalishaji bidhaa yanayotokana na mvua na uvukizaji. Katika shamba la mpunga, maji haya yatakuwa yale ya mvua inayonyesha kwenye shamba hilo na pia kiasi kinachovukizwa.
  • Maji ya bluu yanayotumika katika uzalishaji:haya ni maji yaliyo juu au chini ya ardhi yanayotoka kwenye vyanzo asili au vilivyotengenezwa na binadamu ambavyo hudhibitiwa kwa nyenzo au miundo msingi. Maji haya ndiyo huwa sehemu kubwa zaidi katika bidhaa nyingi. Katika shamba la mpunga, haya ni maji ya kumwagilia mimea yanayotoka kwenye mitaro au kuvutwa kwa pampu.
  • Maji ya kijivu yanayotumika katika uzalishaji: hiki ni kiasi cha rasilimali kinachohitajika kudidimiza athari za uchafuzi uliofanyika wakati wa mchakato wa kuzalisha bidhaa. Katika shamba la mpunga, haya yatakuwa maji yatakayohitajika katika mazingira ili kudidimiza uwepo wa kemikali zilizotumika wakati wa uzalishaji (mbolea, sumu ya mimea, viuadudu, n.k).
water-footprint-coffe-gallons

Maji yanayotumika katika kuzalisha kahawa ni takriban galoni 52 kwa kila kikombe.

Tunawezaje kupunguza kiasi cha maji yanayotumika katika uzalishaji wa bidhaa?

Kauli maarufu ya mwanahisabati na mwanafizikia kutoka Uingereza wa karne ya 19 aliyefahamika kama William Thomson Kelvin inaangazia umuhimu wa kufanya vipimo ili kuboresha mchakato wowote:

“Mara nyingi, mimi husema kwamba ikiwa unaweza kupima unachozungumzia, na kukieleza ukitumia tarakimu, una ufahamu wa jambo hilo; lakini kama huwezi kulipima, ikiwa huweza kulieleza kwa tarakimu, ufahamu wako wa jambo hilo ni mdogo na hauridhishi; huenda ukawa ndio mwanzo wa ufahamu, lakini akilini mwako, huna umaizi mzuri wa Kisayansi wa jambo lolote lile unaloangazia.”

Lodi Kelvin, 1883

Kwa sababu hii, hatua ya kwanza katika kupunguza maji yanayotumika kuzalisha bidhaa kufahamu kuhusu dhana hii na jinsi ya kukokotoa kiasi hicho.

Lakini kuna mapendekezo zaidi ya kusaidia kupunguza maji yanayotumika katika uzalishaji:

  1. Kupunguza matumizi ya bidhaa fulani. Kwa mfano, tule matunda, mboga na vyakula kutoka shambani ambavyo havijahifadhiwa zaidi.
  2. Kutumia bidhaa zinazozalishwa katika maeneo yetu. Kununua vyakula kutoka kwa wakulima wa maeneo yetu hupunguza kiwango cha maji kinachotumika kuzalisha vyakula hivyo kwa namna zisizo za moja kwa moja.
  3. Kutonunua bidhaa zisizo za misimu. Kuhifadhi au kuingiza bidhaa kutoka nchi zingine huongeza kiwango cha maji kinachotumika kuzizalisha.
  4. Zuia kutupa chakula. Nunua bidhaa kwa busara.
  5. Kukuza na kuunga mkono uchumi duara ili kupunguza matumizi na uchafuzi wa maji. Kutumia bidhaa tena na kupunguza matumizi huwa na athari hasi katika kupunguza matumizi ya rasilimali maji.
  6. Kukuza matumizi ya maji ya busara. Kwa mfano, tuache kuogea kwenye hodhi zilizo jaa maji na badala yake tutumie mabafu ya manyunyu.
  7. Kunywa maji ya mfereji. Maji ya chupa yana athari kubwa kwa mazingira kuliko maji ya mfereji.