Kichwa cha makala haya kinafafanua kauli maarufu ya mkemia wa Kifaransa, Antoine Lavoisier katika “Kanuni ya Hifadhi ya Masi” aliyovumbua. Alisisitiza kwamba masi haitengenezwi wala kuharibiwa katika mimemenyuko ya kikemia. Jambo sawia hufanyika kwa maji. Mchakato huu wa mabadiliko unafahamika kama Duru ya Kihaidrolojia.

Hydrological Cycle

Maji ni dutu ambayo molekuli yake ina atomu mbili za haidrojeni na moja ya oksijeni (H2O). Yanabadilika katika hatua tatu: mango, majimaji na gesi. Maji ni muhimu sana katika kuchimbuka na kusitiri maisha ya viumbe na mimea hai mingi duniani. Katika mchakato huu, maji hugeuzwa mara nyingi na yanabadilika kila wakati.

Nguvu ya jua hufanya maji kuvukiza. Baada ya kutoneshwa, kani ya uvutano husababisha kunyesha katika hali ya mvua, barafu au mvua ya mawe. Hali hii inasababisha mzunguko endelevu: Duru ya Kihaidrolojia.

Uhifadhi na Mitiririko ya Maji

Duru ya Kihaidrolojia huwa na michakato miwili mikuu: wa kwanza ni uhifadhi wa maji. Mchakato wa pili ni kutiririsha maji kutoka hifadhi moja hadi nyingine. Baadhi ya mifano ya hifadhi ya maji yaliyo katika hali majimaji ni bahari, maziwa, mawe yanayoshikilia maji chini ya ardhi, mawingu—naam, mawingu! Ingawa watu wengi hudhani mawingu hutengenezwa kwa mvuke, ukweli ni kwamba yana vitone vya majimaji. Katika hali mango, mito ya barafu na theluji ya misimu hukusanya maji. Hatimaye, katika hali gesi, angahewa huhifadhi maji.

Asilimia zifuatazo zinaashiria jinsi maji yanavyogawanywa katika hali tofauti ambazo yanahifadhiwa:

Tunafahamu kwamba kuna maji mengi sana duniani. Hata hivyo, ni asilimia ndogo tu ya maji inayositiri maisha ya viumbe na mimea mingi na kuleta anuwai ya viumbe hai.

water-cycle-distribution-percentage

Usambazaji wa maji

Kwa mpande mwingine, mitiririko inaashiria jinsi maji yanavyohama kutoka duru moja ya uhifadhi hadi nyingine. Baadhi ya mifano muhimu ni kama:

  • Utoneshaji: wakati mvuke wa maji unapopanda kwenye angahewa, unapoa na kuwa majimaji kupitia mchakato wa utoneshaji.
  • Kunyesha: kupitia utoneshaji, mvuke wa maji hugeuka kuwa vitone ambavyo hugeuka kuwa mawingu. Baadaye, maji hunyesha katika hali ya majimaji au mango.
  • Uvukizaji na jumla ya maji mvukizo kutoka ardhini na viumbe hai: maji katika hali majimaji ambayo yamo katika hifadhi kubwa juu ya ardhi kwa kawaida hugeuka kuwa mvuke kwa sababu ya nguvu ya jua. Viumbe hai hutoa mvuke wa maji vinapopumua.
  • Upenyezaji: maji yanayoanguka ardhini kwa kawaida hupenyeza kwenye udongo. Mimea hufyonza sehemu ya maji hayo, sehemu nyingine inavukizwa, na sehemu nyingine inapenyeza hadi kwenye mawe yanayohifadhi maji chini ya ardhi.
  • Maji yanayotiririka juu ya ardhi: baada ya ardhi kulowa, maji hutiririka juu ya ardhi kwa sababu ya kano ya uvutano, na kutengeneza mito.
  • Kuyeyuka: kuyeyuka kwa theluji ya misimu husababisha mitiririko ya maji.

Muda wa wastani ambao maji hukaa katika duru hizi za uhifadhi hujulikana kama muda wa makazi. Unaweza kudumu kwa siku chache hadi mamia ya miaka.

 

Muda wa Makazi:

Ni asilimia ndogo tu ya maji inayositiri maisha ya viumbe na mimea mingi

Kisaidizi Bandiacha Qatium

Usawa wa Maji Kwenye Duru ya Kihaidrolojia

Ingawa duru hii huchukua mkondo sawa kote duniani, kulingana na ukubwa wa vijifumo, vinaweza kutoa au kunasa maji. Kwa jumla, usawa wa maji katika wakati mahususi huzingatia hali yake ya awali, kiasi kilichoingia kwenye duru hiyo, kasoro kiasi kilichotolewa katika mfumo ndani ya wakati huo. Pesa huchukua mkondo sawa: ili kufahamu salio la akaunti fulani, katika wakati mahususi; sharti ufahamu salio la awali pamoja na gharama na pesa zilizochumwa ndani ya kipindi hicho.

Usafi wa Maji

Kulingana na kisa hiki, inawezekanaje kwamba tunapata matatizo ya uhaba wa maji? Sehemu ya jibu lake ni kwamba ni asilimia ndogo tu ya maji inayoweza kusitiri maisha. Wakati wa mchakato wa kutiririka, maji husafirisha dutu zilizochanganyika na maji zilizo katika hali mango, ambazo huenda zikafanya maji yasifae kwa ajili ya kunywewa.

Aidha, ubora wa maji hutegemea michakato asili kwa kiwango fulani. Kwa mfano, michakato hii husababishwa na mmomonyoko wa madini kwenye udongo, kusafirishwa kwa dutu za kioganiki, uvukizaji wa maji kutoka ardhini na viumbe hai, pamoja na michakato ya kimaumbile, kikemia na kibiolojia katika mazingira ya majini, n.k.

Ubora wa rasilimali hii adimu pia hutegemea pakubwa tabia za binadamu. Kwa sababu hii, sharti tuyalinde maji. Ni wajibu wa kila mtu.